Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa Polisi (IPOA) imetuma Timu yake ya uchunguzi katika eneo la Angama Mara Kaunti ya Narok kuchunguza kisa ambapo maafisa wa polisi wanadaiwa kumpiga risasi mtu mmoja.

    Tukio hilo la Alhamisi asubuhi liliripotiwa kusababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa.Vurugu hizo zilizuka baada ya polisi kufyatulia risasi kundi linalodaiwa kuvamia ardhi ndani ya hifadhi ya Angama Conservancy, iliyoko katika kijiji cha Lolkuruk.

    Katika taarifa yake iliyotolewa Ijumaa, Mwenyekiti wa IPOA, Issack Hassan, alithibitisha kupelekwa kwa wapelelezi, akinukuu Kifungu cha 7(1)(a)(x) cha Sheria ya IPOA, ambacho kinatoa mamlaka ya kuchunguza vifo na majeraha mabaya yanayotokana na hatua za polisi.

    Vilevile alituma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa na kuwataka wakaazi wa eneo hilo kuwa watulivu na kuruhusu michakato ya kisheria kutekelezwa.

    June 6, 2025

    Leave a Comment