Radio Osotua › Local News

abunge watoa maoni tofauti kuhusu baadhi ya vipengee vinavyo patikana kwenye mswada wa fedha.

Local News June 14, 2023 Brigit Agwenge

Mjadala wa mswada wa fedha wa mwaka 2023/2024 umeendelea kuibua hisia mseto nchini huku wabunge wakitoa maoni tofauti kuhusu baadhi ya vipengee vinavyo patikana kwenye mswada huo.

Ingawa wabunge wanaounga mkono mswada huo wamekiri kuwa kuna baadhi ya vipengee vinavyohitaji mabadiliko zaidi, wabunge wengi wa upinzani wamekosoa mswada huo na kuutaja kuwa kitanzi kwa wakenya.

Baada ya mjadala kuhusu mswada huo bunge hilo litapiga kura ili kubaini idadi ya wabunge wanaounga mkono na wale wanaoupinga.