Naibu Rais Rigathi Gachagua ameukashifu Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya kwa kutaka kurejeshwa kazini waliokuwa makamishmna wanne wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) walioondoka afisini baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Alisema matakwa ya kuwarejesha Juliana Cherera, Justus Nyang’aya, Francis Wanderi na Irene Masit, Naibu Rais hayawezekani.

DP alisema watatu kati yao walijiuzulu kwa hiari huku mmoja akiondolewa kisheria kupitia mahakama.

Bw Gachagua pia alipuuzilia mbali madai ya viongozi wa upinzani kwamba mgombeaji wao wa urais, Raila Odinga, aliibiwa kura katika kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu mwaka jana huku akimtaka Bw Odinga kustaafu kutoka kwa siasa.

May 6, 2023