Zoezi la kuwahoji mawaziri wateule limeendelea kwa siku ya tatu,seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen akiwa wa kwanza kufika mbele ya kamati inayoendesha zoezi hilo. Murkomen ambaye ameteuliwa kama waziri wa barabara na uchukuzi amesema kuwa miradi mingi ya barabara imesitishwa kutokana na kutolipwa kwa wanakandarasi.Aidha Murkomen amewaonya wanakandarasi ambao hukosa kukamilisha miradi baada ya kulipwa na serikali.

Wa pili kufika kikaangoni  alikuwa ni mwakilishi wa zamani wa kina mama katika kaunti hii ya Narok na ambaye pia ameteuliwa kuwa waziri wa mazingira Soipan Tuya. Soipan amesema kuwa hauchukulii uteuzi wake kama jambo la kawaida ikizingatiwa kwamba amekuwa mwanamke wa kwanza katika jamii ya maa kuteuliwa kama waziri.

Kuhusiana na suala lashamba system lililopendekezwa na naibu rais Rigathi Gachagua, Soipan ameeleza kuwa iwapo ataiidhinshwa,basi wizara ya mazingira itajumuisha maagizo yaliyowekwa katika Sheria ya Usimamizi wa Misitu ya mwaka 2016 ambayo inaruhusu shirika la utunzaji misitu nchini kufanya kazi na jamii zilizo karibu na misitu.

October 19, 2022