Madereva waliosambaza vifaa vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa agosti tisa huko Transmara wameandamana katika makao makuu ya IEBC mjini Kilgoris wakidai malipo yao. Maafisa wa IEBC eneo hilo walitoroka na kufunga afisi zao kutokana na kizaazaa hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari,madereva hao wameeleza kuwa baadhi yao wamelipwa ila sio pesa walizoangana na tume hiyo.Kwa sasa wanamtaka mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kuingilia kati na kutatua tatizo hilo.

October 7, 2022