Chama cha UDA kimeahirisha uchaguzi wa viongozi wa chama hicho uliopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2023. Kupitia taarifa Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala amesema uchaguzi huo utafanyika Aprili 2024.

Malala alibainisha kuwa zoezi hilo liliahirishwa kufuatia kikao cha Baraza la Uongozi la Taifa (BMT) kilichofanyika tarehe 18 Novemba 2023 na kuongozwa na rais William Ruto ambaye ni kinara wa chama hicho. Aliongeza kuwa uchaguzi huo utafanyika katika makundi matatu kuanziaa tarehe 12, 19 na 26 Aprili 2024.

 

November 18, 2023