BY ISAYA BURUGU,21ST JAN 2023-Gavana wa Mombasa  Abdulswamad Shariff Nassir  ameshinda raundi ya kwanza  ya kesi ya kupinga  uteuzi maafisa wakuu kumi  wa serikali ya kaunti waliozinduliwa wiki jana.Hii ni baada ya  mahakama ya leba  kule Mombasa kudinda  kutoa agizo  kuzuia  mchakato wa kuwaidhinisha  maafisa hao wakuu kuanza kutekeleza jukumu lao.

Gavana  Abdulswamad Nassir alikuwa amewateua  mawaziri kumi  katibu wa kaunti ,mkurugenzi  mkuu wa bodi ya huduma kwa umma ya Mombasa  na washauri kadhaa kumsaidia kuongoza.

Hata hivyo  wakaazi wanne wa Mombasa Abdullmajid Ali Busayyid, Mesh Mwaniki, Maria Magdalene Fernandes, na  Mohammed Mohsin Abdulkarim,walikwenda mahakamani  chini ya ombi la dharura wakitaka  kuzuia mchakato wa kuwaajiri maafisa hao.

Wanne hao  kupitia wakili wao  David Maseke wa  Shabaan Associates LLP, walisema gavana huyo alikiuka sheria katika uteuzi huo.

 

 

 

 

 

January 21, 2023