Siku kadhaa  baada ya Waziri  wa uchukuzi  Kipchumba Murkomen kufutilia mbali uteuzi wa generali mstaafu  Joseph Kibwana kama mwenyekiti wa bodi ya almashauri ya Bandari nchini KPA na kumkabidhi wadhifa huo aliyekuwa mbunge wa Kinango   Benjamin Tayari sasa shoka limewangukia wanachama wa bodi hiyo.

Hivi leo,Murkomen amefutilia mbali uteuzi wa wanachama watano na kutaja majina ya watakaojaza nafasi zao.Katika notisi hiyo hiyo iliyochapishwa katika gazeti rasmi la kiserikali, waziri wa afya Susan Wafula, amefutilia mbali  uteuzi wa  Paul Magutu Njaria, Dorcas Wanjiru Ngechu, John Munguti Kisengi, Miriam Wairimu Ndirangu, Stephens Ogutu Oyaya, na  Diana Marion kama wanachama wa bodi ya sumu na dawa nchini.

Mabadiliko hayo yanaanza kutekelezwa kuanzia hivi leo.Vilevile Charles Githinji  ameteuliwa  kuongoza boda hiyo.Uteuzi wa awali wa  James Mandere Rogers Atebe umefutiliwa mbali .Githinji atahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

January 20, 2023