Gavana wa Samburu Jonathan Lelelit amehojiwa na makachero wa DCI mjini Nakuru kuhusu mashambulizi ya mara kwa mara yanayoshuhudiwa katika kaunti ya Samburu.

Hii ni mara ya pili chini ya mwezi mmoja kwa gavana huyo kuhojiwa kuhusiana na ujangili unaoendelea katika kaunti yake.

Aidha akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhojiwa, Lelelit amesema kwamba yeye pia ni mmoja wa waathiriwa wa mashambulizi hayo na ni jukumu la inspekta jenerali wa polisi Japhet Koome na timu yake kuhakikisha kwamba hali ya utulivu inarejea Samburu bali si kumhoji kuhusiana na mashambulizi.

March 5, 2024