By Isaya Burugu,Oct 12,2022- Wasimamzi kutoka  kampuni ya kusaga pareto humu nchini wamezuru kaunti ya Kisii kukutana na gavana Simba Arati kwa lengo la kufufua kilimo cha pareto.MKutano huo wa leo pia umejadili mbinu za kumuinua  mkulima na kutoa mafunzo ya kuboresha zao la pareto na kuimarisha mapato ya zao hilo.

Itakumbukwa kwmaba eneo la Kisii ndilo lililokuwa likikuza zao hilo kwa wingi miaka ya sitini.Wakizungumza na wandishi Habari wakuu  hao  wamewapa matumaini wakulima wa pareto kuwa iwapo wanalenga kuongeza kilimo cha pareto watasaidiwa.

Wakulima hao watasaidiwa kwa mbegu,pembejeo, na msaada mwingine wowote ambao wakulima wangehitaji.

Maeneo ya Bobasi na  Nyaribari masaba  ndio yanayofahamika Zaidi katika eneo hilo la Gusii katika ukusaji wa pareto

October 12, 2022