BY ISAYA BURUGU 8TH DEC 2022-Kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipka nchini IEBC Francis Wanderi  amejiuzulu baada yar ais Wiliam Ruto kumsimamisha kazi Pamoja na makamishna wenzake  watatu.Wanderi  amekuwa kamishna watatu  kujiuzulu  baada ya Justus Nyangaya  na naibu mwenyekiti wa EINC Juliana Cherera.

Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari Wanderi amesema uamuzi huo umesabbaishwa  na ukosoaji usiofaa  ambao anasema umemsababishia fedheha na kutilia shaka maadili yake  kuhudumu katika tume hiyo.

Kamishna huyo  ameonya dhidi ya uamuzi wake kuchukuliwa kumanisha kuwa  amekiri  madai yaliyotolewa dhidi yake.Aidha ameonya  kuwa iwapo mfumo wa usimamizi wa tume hiyo hautashughulikiwa ipasavyo migogoro itaendelea kushuhudiwa.

December 8, 2022