Shakahola 179

Idadi ya watu walioaga dunia katika eneo la shakahola, imefikia 179, baada ya miili 29 zaidi kufukuliwa hii leo.

Idadi hii ndiyo ya juu zaidi kufukuliwa katika eneo hilo tangu zoezi la ufukuzi lilipoanza kwenye msitu huo mwezi jana.

Mratibu wa ukanda wa Pwani Rhoda Onyancha alieleza kwamba maafisa wanaoendeleza shughuli hizo hawakufanikiwa kuwaokoa watu Zaidi hii leo, huku idadi ya watu waliotangazwa kutoweka na wimefikia 609, baada ya watu wengine 15 kuripotiwa kutoweka.

May 12, 2023