Margaret Nyakang'o

Mdhibiti wa bajeti nchini, Margaret Nyakang’o, amepata afueni baada ya Mahakama Kuu nchini kutoa agizo la kusitisha kushtakiwa kwake hadi pale kesi iliyowasilishwa na Mbunge wa Mugirango Magharibi, Mogaka Musyoki, itakapoamuliwa mwezi Mei mwaka kesho.

Musyoki aliwasilisha kesi mahakamani kupinga kukamatwa na kushtakiwa kwa Mdhibiti wa Bajeti, akisema kwamba hatua hiyo ni ukiukaji wa haki zake. Aliongeza kuwa kuna nia fiche katika mchakato wa kumfungulia mashtaka Nyakang’o.

Nyakang’o alikamatwa siku ya Jumanne na kusomewa mashtaka ya uhalifu yanayomhusisha yeye pamoja na watu wengine 10 katika kesi iliyoanza mwaka 2016.

SOMA PIA: Ombi lawasilishwa mahakamani kupinga mashtaka dhidi ya Mdhibiti wa Bajeti

Agizo hilo la mahakama, lililotolewa na Jaji Chacha Mwita, limepokelewa vyema na wabunge kadhaa kutoka ukanda wa Gusii, ambao wameelezea matumaini yao kwamba haki itatendeka kwa usawa.

 

 

December 7, 2023