BY ISAYA BURUGU,8TH DEC 2023-Rais William Ruto hivi leo ameongoza  gwaride la kufaulu kwa zaidi ya wahitimu 10,000 katika chuo cha NYS huko Gilgil.Wahitimu hao wanajumuisha wanaume 6,861, 3,660 na watu wenye ulemavu 47 ambao ni sehemu ya timu iliyoajiriwa Mei mwaka huu. Waajiri hao kutoka kaunti zote ndogo kote nchini wamekuwa wakipitia mafunzo ya kijeshi kwa miezi 6.

Wakati wa hafla hiyo, Mpango wa Urekebishaji Upya wa NYS, chini ya wizara ya utumishi wa umma, utendakazi na usimamizi wa utoaji utatekelezwa.Chini ya mpango huo, NYS itafanywa kibiashara kikamilifu huku mafunzo ya NYS yakiwa hitaji la lazima kwa wafanyikazi wote wa serikali.

Akizungumza katika hafla hiyo waziri wa huduma ya Umma Moses Kuria amewasifu waliofuzu akisema watachangia pakubwa utekelezaji wa ajenda wa serikali. Chini ya mpango huo, vikosi vyenye nidhamu vitakuwa na sharti la lazima kuajiri asilimia fulani kutoka kwa kundi la wahitimu wa NYS miongoni mwa mageuzi mengine.Mikataba ya maelewano kati ya NYS na mashirika mbalimbali ya serikali pia itatiwa saini wakati wa hafla hiyo.

Wakati huo huo rais Wiliam Ruto amesisitiza kujitolea kwa serikali yake katika kubuni mazingira bora ya kuwawezesha vijana kunawiri kimaisha.Akizungumza alipoongoza hafla ya kufuzu kwa wahitimu alfu 10, wa shirika la huduma kwa vijana NYS  huko Gilgil kaunti ya Nakuru,rais amesema katika ulimwengu wa sasa ambao unakumbwa na changamoto nyingi zikiwemo, ugaidi,ukosefu wa ajira na umaskini,vijana wasiokuwa na jukumu la kutekeleza kwa mara nyingi hujipata kwenye mienendo isiyofaa. Hivyo basi rais amesema serikali yake inaendesha mikakati mwafaka ya kuwauzisha vijana katika utekelezaji wa agenda yake ya Botom Up.I

.Aidha rais amesema jukumu la huduma ya vijana kwa Taifa NYS haliwezi kuppuuzwa humu nchini na kwamba seriakli kupitia Taasisi ya NYS itazidi kupanua uwezo wa utoaji mafunzo bora zaidi kwa vijan ahao kuelekea mbele ili kuwaweka katika nafasi nzuri kuhudumia taiafa.

December 8, 2023