Baraza la vyombo vya habari limetangaza kuwa kesho litafanya mkutano na wawakilishi wa sekta ya uandishi wa habari ili kuanzisha mfumo wa kukuza taaluma ya uandishi wa habari.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo David Omwoyo amesema kuwa ongezeko la idadi ya watu wanaojifanya kuwa wanahabari na kuwahadaa wakenya ndio imechochea mkutano huo.

Omwoyo ameongeza kuwa baraza hilo linaendelea kujitolea kukuza mazingira ambayo yanafaa kwa waandishi wa habari kwa kushughulikia masuala muhimu yanayoathiri sekta hiyo.

January 26, 2023