BY ISAYA BURUGU 19TH AUG 2023-Watu sita wameripotiwa kufariki dunia katika kaunti ya Kiambu baada ya kisima walichokuwa wamesimama juu yake kuporomoka.Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, sita hao walikuwa wanatarajia kuhudhuria hafla ya harusi ya mmoja wa rafiki zao katika eneo la Kihunguro, Ruiru na walikuwa wanacheza densi kwa mbwembwe juu ya kisima kilichokuwa kimefunikwa kwa zege ya saruji.Ghafla saruji hiyo iliporomoka na kuwameza sita hao kwenda ndani ya kisima hicho chenye kina cha urefu ambao hadi sasa haujabainika.

Kulingana na polisi, takriban watu 11 walikuwa wakicheza kwenye zege ilipoanguka Jumamosi na wengine wakiokolewa, watu sita walikufa. Mtoto mmoja alikuwa miongoni mwa waliokufa na Waliookolewa walipelekwa katika hospitali ya Ruiru.

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi alithibitisha kisa hicho. Taarifa hizi zinakuja siku chache tu baada ya watu wengine wawili kuripitiwa kufariki katika kaunti hiyo eneo la Thika Kiganjo baada ya kula ugali kutokana na unga waliookota kwenye eneo la kutupwa taka.

Taarifa za awali ziliripoti kwamba wawili hao walifariki hospitalini kutokana na makali ya kukeketwa kwa matumbo na wengine wasiopungua saba walikuwa wamelazwa hospitalini mmoja akiwa katika hali mbaya.

 

August 19, 2023