BY ISAYA BURUGU 27TH DEC 2022-Mwanamme mmoja ambaye ni muhudumu wa bodaboda amesombwa na maji ya mafuriko alipokuwa akijaribu kuvuka mto wakolnkit katika Kijiji cha Ala Lui eneo la kilgoris Transmara magharibi kaunti hii ya Narok.

Hii ni kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa eneo hilo.

Kamanda wa polisi Narok kusini Kzito Mutoro anasema mhudumu huyo ambaye mwili wake umepatikana jioni ya leo inarifiwa alikuwa akijaribu kuvuka mto huo uliyokuwa umefurika siku ya krismasi alikuwa akijaribu kutoka upande wa kilgoris kuelekea migongo akitumia barabara ya kilgoris kuelekea Migingo lakini akazidiwa na maji na kusombwa.

Vilevile Mutoro anasema hakuna aliyekwenda kuandikisha taarifa kwa polisi hadi hiyo jana ambapo pikipiki ya marehemu ilipatikana  eneo la jamhuri.

Kmanda huyo wa polisi amewaimiza wananchi kuwa wangalifu wanapovuka mito iliyojaa haswa wakati huu ambapo mvua kubwa inaendelea kushudiwa.

 

December 27, 2022