Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC imeweka mipango inayofaa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mtaala mpya wa CBC unaendeshwa kama ilivyoratibiwa.

Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Nancy Macharia amesema mwaka ujao Zaidi ya walimu alfu 30 watatumwa kote nchini kusaidia katika kufanikisha azimio hilo wakiwemo wale walio kwenye mafunzo.

Walimu hao wakitarajiwa kupiga jeki mpango wa kuwafunza wanafuzni wa kiwango cha ngazi ya chini ya  secondari.

Pia amewataka  walimu waliohitimu kutuma maombi ya kazi katika dirisha la sasa la kuwaajiri walimu alfu 30.Tarehe ya mwisho kutuma maombi itakuwa tarehe 23 mwezi huu.

December 21, 2022