Radio Osotua › Local News

Naibu Rais asuta zoezi la kukusanywa kwa sahihi za kumbandua rais mamlakani.

Local News July 8, 2023 Brigit Agwenge

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesuta hatua ya kinara wa Azimio Raila Odinga ya kuanzisha zoezi la kukusanya sahihi katika azma ya kumbandua mamlakani Rais William Ruto.

Odinga alitangaza hatua hiyo ya kukusanya sahihi milioni 10 hapo jana wakati wa maandamano ya Saba Saba.

Akizungumza katika kijiji cha Giaituu, eneo bunge la Mathira, Gachagua alisema uchaguzi hauamuliwi kwa sahihi bali kwa upigaji kura huku akimeleza Odinga kusubiri hadi ucahguzi ujao iwapo anataka kuwania urais.