Radio Osotua › Local News

Nancy Kigunzu almaarufu Mathe wa Ngara ataka kujua zilikopelekwa shilingi Ksh.13.4M ambazo polisi walimpata nazo.

Local News August 28, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU 28TH AUG 2023-Nancy Kigunzu almaarufu Mathe wa Ngara sasa anataka kujua Ksh.13.4M ambazo polisi walimpata nazo zilipelekwa wapi.

Kupitia kwa mawakili wake Danstan Omari na Cliff Ombeta, Mathe wa Ngara anasema kuwa pesa hizo zinafaa kuwa kielelezo na hazikupaswa kukamatwa na serikali.

Katika majibu yake, upande wa mashtaka ulisema pesa hizo zinaweza kutaifishwa.

Wakati wa uvamizi katika jengo linaloaminika kuwa la Kigunzu, polisi walisema walinasa mamilioni na dawa za kulevya.

Ijumaa iliyopita Mahakama Kuu iliamuru Ksh.13.4 milioni zitunzwe kwenye akaunti ya uhifadhi ya Mali na Urejeshaji (ARA) katika Benki ya Biashara ya Kenya.