Radio Osotua › Local News

NCCK lamtaka rais William Ruto kufanya mazungumzo na Raila Odinga ili kusitisha maandamano.

Local News March 23, 2023 Brigit Agwenge

Baraza la madhehebu mbalimbali nchini NCCK limemtaka rais William Ruto kufanya mazungumzo na kinara wa upinzani Raila Odinga ili kusitisha maandamano.

Wakiwahutubia waandishi wa habari huko Limuru, viongozi hao wameeleza kuwa kuna haja ya kutumia njia mbadala ya kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakumba wakenya badala ya maandano.

Hali kadhalika wamemtaka Odinga kutumia njia zilizoainishwa katika Katiba na Sheria za Kenya kabla ya kuchukua hatua kubwa wakidai kuwa maandamano yatawaongezea wakenya matatizo.