Ndindi Nyoro

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati bunge la kitaifa kuhusu maswala ya Bajeti na Matumizi ya fedha.

Katika wadhifa huo, Ndindi atakuwa na uwezo wa kuwaalika wawakilishi wa kamati za idara mbalimbali kutoa mapendekezo yao kuhusu yale wangetaka yaorodheshwe katika bajeti. Naibu Mwenyekiti wa Ndindi atakuwa Mary Emaase, ambaye alimshinda Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, katika kinyang’anyiro kikali kwenye kikao cha bunge hilo alasiri ya leo wawili hao wakitarajiwa kuongoza kamati hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Katika taarifa sawia ni kuwa mbunge mteule John Mbadi alichaguliwa bila kupingwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya uhasibu katika bunge la kitaifa (PAC) katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo.

November 3, 2022