Na hali ya sintofahamu imeanza kushuhudiwa katika chama ch Jubilee, baada ya sehemu ya wabunge walio wanachama wa chama hicho, kuandaa kikao na Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua katika ikulu Mapema leo.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Pamoja na mbunge mteule Sabina Chege, mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Kanini Kega. Katika taarifa yake baada ya kikao hicho, Rais alisema kuwa taifa linawahitaji viongozi wote ili kuweza kupiga hatua mbele.

Hata hivyo katibu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni, ameeleza kuwa chama hicho hakiwezi kufanya kazi na serikali ya Rais William Ruto. Kioni alikua akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Muungano wa Azimio katika uwanja wa Kamukunji.

January 23, 2023