Radio Osotua › Local News

Rais Wiliam Ruto asema wakati wakupiga siasa umekwisha, ni wakati wa kuwahudumia wananchi

Local News April 22, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,22ND APRIL,2023-Rais  William Ruto yuko  Igembe kaskazini , kaunti ya Meru kuzindua ukarabati wa barabara ya  Kaelo-Kamukunji-Mutuati  kufikia kiwango cha kisasa.

Rais ni mgeni wa gavana  Kawira Mwangaza miongoni mwa viongozi wengine akiwemo Waziri wa kilimo  Mithika Linturi.Akiwahutubia wenyeji , Ruto amechukua fursa hiyo kuwashukuru kwa kupigia kura kwa wingi serikali ya Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.Vilevile rais   ameunyoshea upinzani  kidole cha lawama  haswa kinara wake Raila Odinga kutokana na kile alichosema ni njama yake kutaka kuendeleza siasa bila kuzingatia kuwa sasa ni wakati wa kuwahudumia wananchi.

.Rais amesema amejitolea kuhakikisha kuwa miradi ya barabara imekamilika kwa wakati ili kuhakikisha uchui wa taiafa unainuka .Ruto amesema  atahakikisha barabara aliyozindua imekamilika na atarejea Meru mwezi disemba kushuda kukamilika kwake

.