BY ISAYA BURUGU 28TH APRIL,2023-Rais Wiliam Ruto amesema kuwa serikali yake imejitolea kuboresha Maisha ya kila mwananchi.

Akizungumza alipozindua ukarabati wa barabara ya kilomita 65 mjini Ongata Rongai,rais amesema barabara bora ndizo zitakazowawezesha wakulima kusafirisha mazao yao hadi sokoni na kupata faida.

Rais ameahidi kuwa bei ya unga itashuka Zaidi kufikia juma lijalo.Rais ameusuta upinzani kwa kuendelea kutatiza mstakabali wa serikali kuwatekelezea wananchi kazi.

Rais ametangaza kuwa hivi karibuni atazindua awamu ya pili ya ujezni wa nyumba za makaazi za gharama nafuu katika eneo hilo.

 

April 28, 2023