Rais William Ruto sasa amemteua Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla kuwa Mkuu mpya wa Majeshi, akichukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi ambaye muda wake wa kuhudumu umefikia kikomo.

Jenerali Ogolla alikuwa, akihudumu kama Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.

Jenerali Kibochi, kulingana na waraka kutoka Wizara ya Ulinzi, anaondoka baada ya kutumikia jeshi kwa miaka 44.

Rais Ruto, katika mabadiliko hayo ya kijeshi, pia alimpendekeza Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Kitaifa Luteni Jenerali Jonah Mwangi kuchukua wadhifa wa zamani wa Jenerali Ogolla kama naibu mkuu wa majeshi na Kisha akampandisha cheo Meja Jenerali Said Farah kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Taifa.

April 28, 2023