Rais William Ruto amefanya mazungumzo na rais wa Israel Isaac Herzog nchini Isarel ambapo wawili hao wameafikiana kushirikiana hasa katika ukuzaji wa chakula.

Rais Ruto vilevile ameelezea hamu yake ya kushirikiana na taifa hilo kwenye sekta za afya, uchumi wa baharini pamoja na usalama ikizingatiwa kuwa Kenya inasaidia katika mazungumzo ya kurejesha amani katika mataifa mbalimbali.

wakati wa mkutano wake na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu,wawili hao wameeleza kuwa Kenya na Israel zitashirikiana kuondoa vikwazo vya kibiashara kati yao.

Alisema kutokuwepo kwa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Kenya na Israel ni “kizuizi kikubwa” ambacho kinaendelea kutatiza biashara na utalii.

Aliona kuwa Kenya na Israel zina vivutio vya kipekee vya kimataifa ambavyo vinaweza kuendeleza ukuaji thabiti wa utalii.

Kwa upande wake, Bw Netanyahu alijitolea kuendelea kufanya kazi na Kenya katika kupambana na ugaidi, kukabiliana na itikadi kali.

.

May 9, 2023