BY ISAYA BURUGU 13TH MAY 2023-Rais Wiliamu Ruto na kinara wa Azimio la umoja one Kenya Raila Odinga wamekutana ana kwa ana leo   tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.Viongozi hao wawili wamekutana katika hafla ya mazishi ya Marehemu Mukami Kimathi, mke wa aliyekuwa mpiganaji wa Mau Mau nchini Kenya Dedan Kimathi anayezikwa leo  Mei 13 nyumbani kwake kaunti ya Nyandarua.

Kando na Rais Ruto na Odinga ,viongozi wengine waliofika ni pamoja na naibu rasi Rigathi Gachagua na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi miongoni mwa watu wenye haiba ya juu katika siasa za Kenya ambao wanahudhuria mazishi hayo.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Odinga kukutana uso kwa uso na Ruto na naibu wake ambao wamekuwa wakizozana kwa maneno makali ya lawama takribani mwaka mmoja tangu kukamilika kwa uchaguzi uliokuwa na ushindani wa aina yake kati ya pande hizo mbili.

May 13, 2023