Radio Osotua › Local News

Serikali kujenga shule tano maalum chini ya Mpango wa Amani katika kaunti ya pokot magharibi.

Local News June 9, 2023 Brigit Agwenge

Waziri wa usalama wa ndani na Utawala wa Kitaifa Kithure Kindiki ametangaza kuwa serikali itajenga shule tano maalum chini ya Mpango wa Amani.

Shule hizo tano Dira, Todo, Tuwit, Lomuke, na Chepchoren, zitahakikisha wanafunzi kutoka Kaunti za Elgeyo Marakwet, Baringo na Pokot Magharibi wanapata mafunzo ili waweze kubadili vizazi vijavyo na kueneza amani na utangamano katika kaunti hizo ambazo zinashuhudia mapigano ya mara kwa mara kufuatia wizi wa mifugo.

Kindiki ameeleza kuwa utangamano wa wanafunzi kutoka jamii hizo utapunguza uhasama.