Idara ya afya ya katika kaunti ya Bomet imesema kwamba iko katika hali ya kutahadhari baada ya kisa cha ugonjwa wa Kipindupindu kuthibitishwa katika kaunti hiyo, huku mgonjwa aliyepatikana na ugonjwa huo akitengwa katika hospitali ya misheni ya Litein.

Kulingana na Waziri wa afya katika kaunti hiyo Dkt Joseph Sitonik, watu wengine 18 walio na dalili sawia wanahudumiwa katika vituo mbalimbali vya matibabu katika kaunti za Bomet na Kericho.

Zaidi ya hayo, Dkt. Sitonik amesema kuwa watu walioathiriwa walikuwa sehemu ya wanafamilia kutoka Kaunti ya Bomet waliohudhuria harusi huko Kitengela, Kaunti ya Kajiado, wiki moja iliyopita.

December 17, 2022