Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa Polisi IPOA imejibu matamshi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome ambayo yaliiweka kati ya ‘mashirika yenye shughuli nyingi’ inayojihusisha na masuala ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, mwenyekiti wa IPOA Anne Makori pia amemkashifu Koome kwa kuwaeleza maafisa wa polisi kutumia bunduki dhidi ya washukiwa wa uhalifu.

Makori ameongeza kuwa mamlaka hiyo kwa miaka 10 iliyopita imekuwa na shughuli nyingi kuhakikisha kuwa maafisa waliopewa jukumu la kulinda maisha na mali ya Wakenya wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Aidha ameeleza kuwa maafisa wengi ndani ya NPS wanafuata sheria, ikibaini kuwa kati ya malalamiko 20,000 dhidi ya polisi ni faili 500 pekee ambazo zimetumwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma na mapendekezo ya kushtakiwa.

December 17, 2022