Ukosefu wa miundombinu muhimu hasa katika sekta ya usafiri miongoni mwa mataifa ya Afrika, ni mojawapo ya changamoto zinazochangia katika ongezeko la bei za bidhaa kati ya mataifa haya kwa hadi asilimia 40.

Haya ni kwa mujibu wa Rais William Ruto, ambaye amesema kwamba tatizo la mkurupuko wa bei za bidhaa itapungua na biashara kati ya mataifa ya afrika kuimarika iwapo kutakua na miundombinu mwafaka hasa ya usafiri. Rais alikua akizunumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la uwekezaji humu nchini mapema.

Aidha rais alieleza umuhimu wa vikao vya aina hii, katika kuinua uchumi wa mataifa mbalimbali barani Afrika hasa yaliyo mbali na bahari.

May 29, 2023