Mark Mwenje

Muungano wa Azimio la Umoja umemteua Mark Mwenje ambaye ni mbunge wa Embakasi Magharibi kama naibu wa mnadhimu katika bunge la kitaifa, kutwaa wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na mbunge mteule Sabina Chege.

Mabadiliko haya yametangazwa na kinara wa wachache katika bunge la taifa Opiyo wandayi alasiri ya leo. Katika taarifa yake, Wandayi amewasuta viongozi wa Jubilee wanaounga mkono serikali, akiwataka kuelekea debeni kwa uchaguzi iwapo wanania ya kugura muungano huo.

Katika taarifa ya muungano huo kwenye kikao na wanahabari alasiri ya leo, Mbunge huyo pia alisuta uongozi wa Kenya Kwanza kwa kile alichokitaja kama juhudi za kumaliza utawala wa vyama vingi nchini.

Wandayi aidha alitangangaza kuwa muungano wa Azimio hautanedelea na mazungumzo ya pande mbili, kwani haujaridhika na hatua zilizopigwa na Serikali kuwaepusha wakenya na gharama ya juu ya maisha. Pia upinzani umeahidi kutumia njia zozote katika kuupinga mswada wa fedha unaoependekezwa na serikali, akisema kwamba mapendekezo yaliyopo yatawaumiza wakenya.

 

May 30, 2023