BY ISAYA BURUGU 2ND MARCH,2023-Ukosefu wa usalama umeonekana kukidhiri katika baadhi ya sehemu kaunti ya Garissa   huku kamati ya usalama eneo hilo ikikutana na viongozi wakidini kusaka mbinu za kukomesha ugaidi.

Kamishna wa kanda ya kaskazini  mashariki John Otieno amewataka viongozi hao wakidini kutumia ushawishi wlaio nao katika jamii kutambua na kurekebisha mienendo isiyofaa.

Otieno amesema serikali haitakubali vikundi vya kigaidi kutatiza mipango yakimaendeleo ya serikali na kuonya kuwa yeyote atakayepatiikana atakabiliwa kisheria.Viongozi hao wakidini walikubali kushirikiana na serikali kuwaelekeza waumini makanisani na misikitini.

 

 

 

 

March 2, 2023