Radio Osotua › Local News

Wanachama wa kamati ya kuwateua makamishna wa IEBC waapishwa.

Local News January 27, 2025 Brigit Agwenge

Wanachama wa kamati iliyoteuliwa na rais William Ruto asubuhi ya leo kuwapiga msasa na kuwateua makamishna wa IEBC akiwemo mwenyekiti wa tume hiyo wameapishwa.

Walioapishwa ni Prof. Adams Oloo, Dk. Nelson Makanda, Fatuma Saman, Amb. Koki Muli, Evans Misati, Nicodemus Bore Kipchirchir, Andrew Tanui Kipkoech, Carolene Kituku na Linda Kiome Gakii.

Katika notisi ya gazeti la serikali ya Januari 27, 2025 rais alibatilisha uteuzi wa wajumbe wa jopo hilo ambao waliteuliwa mapema 2023.

Kwenye hotuba yake, jaji mkuu Martha Koome ambaye aliongoza hafla ya kuapishwa kwa wanakamati hao, aliwataka kudumisha uadilifu wakati wa zoezi la kuwapiga msasa makamishna watarajiwa, akisema kuwa IEBC ni kiuongo muhimu katika uchaguzi wa Kenya.