Huku gumzo la vyakula vya kisaki au GMO likiendelea kutawala na kauli zikitolewa kutoka pande mbalimbali, wazee wa Njuri ncheke kutoka katika kaunti ya Meru, wamejitokeza na kuiunga mkono hatua ya serikali ya kuagiza vyakula hivi vya GMO.

Wazee hao wameweka wazi kuwa wana imani na serikali ya rais Ruto wakieleza kuwa serikali itafanikisha ajenda yake ya kutoa chakula cha bei nafuu kwa wananchi wote, wakiongeza kuwa semi za kupinga hatua hii zinatolewa na upinzani ili kujitafutia uaarufu wa kisiasa.

Kwa upande mwingine magavana nchini kupitia baraza la magavana wamejitokeza na kupinga hatua ya serikali ya kuagiza vyakula vya GMO bila mashauriano na washikadau wengine au hata wananchi

November 23, 2022