Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ametoa msimamo wake kuhusu utata unaozunguka hatua ya serikali kuruhusu uingizaji wa vyakula kisaki humu nchini.

Kwenye kikao na waandishi wa habari, askofu Muheria ameyasuta matamshi ya waziri wa biashara na viwanda Moses Kuria kuhusu vyakula hivyo na kuitaka serikali kufanya mazungumzo na wataalam wa chakula na kilimo ili kupata suluhu bora kabla ya kuidhinisha kikamilifu matumizi ya vyakula hivyo.

Msimamo wa askofu Muheria unajiri siku moja tu baada ya kinara wa azimio Raila Odinga kupinga uingizaji wa tani kumi za mahindi ya GMO ambazo tayari zimeagizwa na serikali.

November 21, 2022