Naibu wa rais Rigathi Gachagua amempongeza Naibu chansela wa chuo kikuu cha Kenyatta Paul Wainaina kwa kutopatiana kipande cha ardhi cha chuo hicho kwa serikali ya aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufuzu kwa mahafali 5,500 wa chuo hicho, Gachagua amesema kuwa licha ya kudhalilishwa na kusimamishwa kazi, chansela huyo hakulegeza kamba katika msimamo wake.

Aidha Gachagua ameongeza kuwa serikali ya Kenya kwanza haitowadhalilisha wakuu wa vyuo bali itawalinda na kuzingatia matakwa yao.

December 16, 2022