Joseph Kuria Irungu maarufu Jowie amehukumiwa kifo kwa kosa la kumuua mfanyabiashara Monica Kimani mwaka wa 2018.

Akitoa hukumu hiyo, jaji wa mahakama kuu jaji Grace Nzioka amesema kuwa mauaji ya Kimani yalikuwa yamekusudiwa.

Aidha jaji Nzioka alibainisha kuwa upande wa mashtaka, katika mawasilisho yake, uliiomba mahakama kumhukumu kifo Jowie kwa madhara aliyosababisha kwa familia ya mwathiriwa

Aliongeza kuwa Jowie kwa mawasilisho yake aliomba msamaha kwa familia ya Kimani na kutumai kwamba marehemu atapumzika Amani.

Mwezi uliopita Jowie alipatikana na hatia ya mauaji ya Monica Kimani, aliyeuawa kikatili katika nyumba yake ya Lamuria Gardens jijini Nairobi usiku wa Septemba 19, 2018.

March 13, 2024