Wahudumu wa magari na bodaboda nchini wamepata afueni baada ya mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli (EPRA) kutangaza punguzo la bei kwa bidhaa za petroli.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo hii leo, bei ya Super Petrol itapungua kwa Ksh.7.21, Dizeli kwa Ksh.5.09 na Mafuta ya Taa kwa Ksh.4.49.

Kufuatia ukaguzi huo, lita moja ya petroli jijini Nairobi itauzwa kwa Ksh.199.15, dizeli kwa Ksh.190.38 na Mafuta ya Taa kwa Ksh.188.74.

Bei hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia saa sita usiku, Machi 15 hadi Aprili 14, 2024.

March 14, 2024