Kampuni za mawasiliano kama vile Safaricom na Airtel  zimeagizwa kufunga laini za simu ambazo hazitasajiliwa katika siku 60 zijazo katika hatua ya kutekeleza uzingatiaji wa zoezi la usajili lililofungwa Jumamosi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumatatu, Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) imeruhusu dirisha la miezi miwili zaidi ili kuhakikisha kwamba zoezi la usajili linafuatwa kwa asilimia 100. Mwishoni mwa kipindi cha siku 60, mdhibiti wa sekta ya mwasiliano na teknolojia anatarajiwa kufanya ukaguzi ili kujua kiwango cha uzingatiaji.

October 17, 2022