Matokeo ya watahiniwa wa gredi ya sita watakaojiunga na ngazi ya chini ya sekondari mwaka ujao yatakuwa tayari kwenye mtandao wa KNEC kufikia tarehe 16 mwezi januari.

Kila mwanafunzi aliyeandika mtihani huo atapokea matokeo yake binafsi huku kila shule pia ikipokea matokeo yake.

Aidha kutakuwa na ripoti ya kitaifa kwenye mtandao huo wa KNEC ambayo itaonyesha jinsi wanafunzi walivyofanya kwenye kila somo na kubaini masomo yanayohitaji bidii Zaidi.

Hali kadhalika matokeo hayo hayatatumiki kuwasajili wanafunzi katika ngazi ya chini ya sekondari.

December 21, 2022