Haji

Idara ya ujasusi nchini Ilitoa taarifa kuhusu matukio katika msitu wa shakahola kwa muda unaofaa.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu mteule wa huduma ya ujasusi nchini Noordin Haji, ambaye aliitetea NIS dhidi ya tuhuma kuwa ilizembea katika utoaji wa taarifa kuhusu matukio ya kusikitisha yaliyosababisha zaidi ya vifo vya wakenya 200 kwenye kaunti ya Kilifi.

Haji ambaye alihudhuria kikao cha bunge ili kupigwa msasa, alieleza kwamba ofisi ya ODPP iliwashtaki baadhi ya wahusika kama vile Paul Makenzi ila idara ya mahakama iliwatoza faini ya chini washukiwa, jambo ambalo lilitatiza uchunguzi zaidi kutoka kwa idara za usalama.

 

May 30, 2023