Muungano wa madaktari nchini KMPDU umeendelea kumkashifu waziri wa afya Susan Nakuhmicha kwa kupendekeza kupunguzwa kwa mishahara ya madaktari wanagenzi kinyume na ilivyoainishwa kwenye mkataba wa maelewano wa mwaka 2017.

Wakiwahutubia waandishi wa habari jijini Nairobi,muungano huo umeeleza kuwa mshahara ambao wanagenzi wanapokea kwa sasa uliidhinishwa na tume ya kuratibu mishahara ya wfanyakazi wa umma SRC wakati wa utiaji saini wa CBA.

Mgomo wa madaktari umeingia siku ya 22 hii leo.

Wakati huohuo katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amewasihi madaktari wanaogoma kurejea kazini huku mazungumzo yakiendelea.

Akizungumza kwenye warsha ya siku tatu ya wahudumu wa afya wa kujitolea katika kaunti ya kisumu, bi. Muthoni amesema kuwa wako tayari kufanya mazungumzo tena na madaktari ili kutafuta suluhu la kudumu kuhusu changamoto zinazowakumba.

Aidha amewarai madaktari kufanya mazungumzo bila vikwazo ili kukwamua mazungumzo yaliyosambaratishwa

Kuhusu suala la wahudumu wa afya wa kujitolea, Muthoni amesema kuwa serikali imetoa shilingi bilioni 6.2 inayotumika kuwalipa wahudumu hao

April 4, 2024