Ruto Kuria

Rais William Ruto hii leo ameliongoza taifa katika maombi ya Kitaifa katika hoteli ya safari park jijini Nairobi.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja viongozi kutoka katika nyanja mbalimbali za kisiasa, ingawa viongozi wa upinzani kutoka muungano wa Azimio La Umoja One hawakuhudhuria.

Rais William Ruto alitumia fursa hiyo kupigia upatu matozo ya asilimia tatu ya nyumba akidai kuwa fedha hizo zitawahakikishia wakenya ajira.

Vilvile kwa mara nyingine rais Ruto amesema kwamba uchaguzi wa mwaka jana uliompa ushindi, ulikuwa uchaguzi ambao ulikaidi misingi ya kikabila ambayo amedai kuwa hufafanua siasa za humu nchini kila wakati.

June 7, 2023