Wakenya wapatao 240,000 katika kaunti ya Narok wanakumbwa na makali ya njaa baada ya kushuhudiwa kwa vipindi virefu vya jua na ukame unaokumba kaunti 23 kote nchini. Ni kutokana na hali hii ambapo viongozi wa serikali ya kaunti ya Narok wakiongozwa na gavana Patric Ole Ntutu pamoja na viongozi wa sekta mbalimbali katika kaunti ya Narok wameanzisha juhudi za kuwasaida wananchi kukabiliana na makali ya njaa. Gavana Ntutu pamoja na kamishena wa Narok Bw.Isaac Masinde wameongoza kikao cha kujadili mbinu mwafaka za kuwasaidia wananchi walio katika hatari zaidi.

Akiwahutubia waandishi wa habari nje ya Ofisi yake kamishena Isaac Masinde amesema zaidi ya shule 130 katika kaunti ya Narok zinahitaji msaada wa chakula kutokana na makali ya njaa. Masinde amesema kuwa serikali kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali wanafanya juhudi  za pamoja ili kuhakikisha kuwa wamesamabaza chakula cha msaada kwa maeneo yaliyoathirika. 

Gavana Ntutukwa upande wake amesema kuwa sehemu zilizokabwa zaidi na njaa ni maeneo ya Mosiro Narok mashariki, Narosura, maji moto, eneo la Loita, Naikara, kapsasian eneo la Ilkeren Trasmara magharibi pamoja na eneobunge la Emurua Dikirr. Ntutu amesema serikali ya kaunti ya Narok itashirikiana na ile ya kitaifa kuhakikisha kuwa misaada mbali mbali imewafikia wakazi wa maeneo haya. 

Taarifa zaidi

Watu 6 Waangamia Kwenye Ajali ya Barabara Eneo la Silanga, Narok

Watu sita wameaga dunia na wengine saba kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea eneo la Silanga…

Mkuu wa Majeshi Jenerali Francis Ogolla Kuzikwa Siku ya Jumapili Familia Yasema.

Aliyekuwa Mkuu wa majeshi humu nchini Marehemu Jenerali Francis Ogolla, ambaye alifariki katika ajali ya ndege katika kaunti…

Askofu mkuu Maurice Muhatia ateuliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la maaskofu KCCB.

Askofu mkuu wa jimbo kuu la Kisumu Maurice Muhatia Makumba ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa…

October 11, 2022