Rais Wiliam Ruto hii leo ameliongoza taifa kuadhimisha siku kuu ya jamhuri ya 59.Sherehe hizo ambazo ziliandaliwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi ziliangazia teknolojia na ubunifu humu nchini.

Kwenye hotuba yake, rais Ruto amesema kuwa ajenda ya serikali ya kwanza ni kukabiliana na changamoto ya gharama ya maisha kwa kuhakikisha wakulima wanapata mbolea ya bei nafuu huku akiweka wazi kuwa serikali itaagiza magunia milioni 10 ya vyakula vya aina mbalimbali.

Kama njia mojawapo ya kuwawezesha wakulima kupata mbolea bila changamoto zozote, rais Ruto ameeleza kuwa serikali inanuia kutumia teknolojia kusambaza bidhaa hiyo kwa wakulima kote nchini.

Kuhusiana na suala la ajira kwa vijana, Ruto amedokeza kuwa vijana 11,000 waliokuwa wamesajiliwa chini ya mpango wa kazi mtaani, wataajiriwa kupanda miti milioni 1.5 jijini Nairobi ili kuongezea kiwango cha msitu nchini.

 

December 12, 2022