Serikali imepata pigo jingine baada ya Mahakama kuu kusitisha hatua ya kupelekwa kwa maafisa wa polisi 1,000 nchini Haiti, ikisema hatua hiyo ni kinyume cha sheria.

Akitoa agizo hilo , jaji Chacha Mwita, alisema baraza la usalama la kitaifa halina mamlaka ya kuwapeleka maafisa wa polisi kuhudumu nje ya nchi.Jaji Mwita aliongeza kuwa baraza hilo la usalama la kitaifa limeruhusiwa tu kupeleka vikosi vya ulinzi KDF, kudumisha amani katika nchi za nje.

Hatua ya kuwapeleka maafisa wa polisi nchini Haiti, ilipingwa mahakamani na Chama cha wanasheria nchini pamoja na kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot.

Kenya ilijitolea kuongoza kikosi cha maafisa wa polisi wa kimataifa kudumisha amani nchini Haiti mwezi Septemba mwaka 2023, baada ya Haiti kuomba msaada wa polisi wa kimataifa, kurejesha hali ya utulivu nchini humo.

January 26, 2024