KMPDU Doctors-one-month-ultimatum-over-comprehensive-medical-insurance

Muungano wa Wahudumu wa Afya na Matabibu wa Meno nchini (KMPDU) umetoa ilani ya kuandaa mgomo wa kitaifa kuanzia mwezi Machi, kufuatia kuondolewa kwa ufadhili wao uliokuwa katika mpango wa bima ya Afya NHIF. Kupitia waraka uliotumwa kwa Wizara ya Afya, KMPDU imeeleza malalamiko yao na kudai kurejeshwa kwa marupurupu ya afya kwa wanachama wao.

Katika waraka huo uliosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa KMPDU, Dennis Miskellah, muungano huo umetilia mkazo hitaji la kurejeshwa kwa marupurupu hayo baada ya serikali kufuta mpango wa bima wa NHIF na kuanza kutumia mpango wa Afya ya Jamii chini ya Bima ya Huduma za Afya (SHIF).

SOMA PIA :Punda Amechoka! KMPDU yaitaka serikali kuwaajiri matabibu zaidi.

Bwana Miskellah anaeleza kwamba wahudumu wa afya walikuwa na uwezo wa kupokea huduma za matibabu katika hospitali yoyote nchini, jambo ambalo hawajahakikishiwa katika bima mpya. Aidha ameongeza kuwa kuondolewa kwa ufadhili wao huenda kukalemaza uwezo wa matabibu kupokea huduma wanazotoa kwa wagonjwa hospitalini

Kando na lalama hizo, KMPDU imeitaka Bima ya SHIF kutumia sajili ya watoa huduma walioidhinishwa hapo awali na NHIF badala ya kuanzisha usajili mpya.

 

January 29, 2024