Mkuu wa Mawaziri na ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni, Musalia Mudavadi amesema kuwa serikali itahakikisha wakenya wanaoishi nje ya nchi hawadhalilishwi katika mataifa hayo ya kigeni.

Mudavadi amesema Kenya haitalegea katika juhudi zake za kuwalinda watu wake popote walipo na kwamba serikali itapeleka zana zake za kidiplomasia kwa ajili hiyo.

Aliyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasmi Wizara ya Masuala ya Kigeni na Diaspora jijini Nairobi. Mudavadi anachukua wadhifa huo kutoka kwa Alfred Mutua aliyehamishwa hadi katika wizara ya Utalii na Wanyamapori.

Share the love
October 17, 2023